GUINEA-AMNESTY-SIASA-USALAMA

Amnesty International yalaani ukandamizaji wa kisiasa nchini Guinea

Oumar Sylla, naibu mratibu wa muungano wa mashirika ya kiraia nchini guinea na kiongozi wa vuguvugu llinalodaia kulinda Katiba ya nchi, FNDC, ametimiza miezi mitatu jana Ijumaa Julai 17 akizuiliwa jela.

Waandamanaji wakipinga kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba wakikabiliana najeshi huko Conakry, Machi 22, 2020.
Waandamanaji wakipinga kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba wakikabiliana najeshi huko Conakry, Machi 22, 2020. CELLOU BINANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International linalaani kizuizi hicho kisichofuata sheria dhidi ya mawanaharakati huyo.

Oumar Sylla alikamatwa baada ya kuzungumza katika kipindi cha redio Aprili 17. "Alikuwa ameitisha maandamano, lakini hasa alikuwa amelaani mauaji, vitendo vya mateso, kuzuiliwa kiholela na kunyanyasawa kwa wanaharakati kadhaa wa wanaunga mkono demokrasia, katika mji wa Nzérékoré.

Wakati wa mahojiano hayo kwenye redio, pia aliwahusisha maafisa wa serikali katika vitendo hivyo ”, amebaini Kiné-Fatim Diop, afisa wa kampeni kwa shirika la Amnesty International katika kanda ya Afrika Magharibi katika mahojiano na Jeanne Richard, wa kitengo cha RFI Afrique.

Wiki moja baadaye, Oumar Sylla alishtakiwa kwa "kutoa habari za uwongo". "Kuzuiliwa kwake, kwetu, ni katika mfumo wa mkakati wa mamlaka, ambayo inanyanyasa wanaharakati wote na kujaribu kunyamanzisha sauti zote zinazopinga Katiba mpya, ambayo inabadilisha idadi mihula ya rais kwenye uongozi wa nchi na ambayo inamuwezesha Rais Alpha Condé kuwania tena katika uchaguzi ujao, kwa mara ya tatu mfululizo, " amesema Kiné-Fatim Diop.

Tangu Mei 7, mwanaharakati mwingine wa FNDC, Saïkou Yaya Diallo, alihukumiwa kwa makosa ya "dhuluma, vitisho na matusi hadharani". Shirika la kimataifa la Amnesty International pia limetoa wito wa mwanaharakati huyo kuachiliwa huru.