Mali: Wataalam wa ECOWAS wapendekeza M5 kujiunga na serikali ya umoja
Upinzani nchini Mali na ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wamekutana kwa mara ya 4 Ijumaa wiki hii, Julai 17 kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini Mali.
Imechapishwa:
Wataalam wa jumuiya hiyo ya kikanda wametoa mapendekezo kwa upinzani hasa kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itaanzisha mageuzi ya kisiasa na mashtaka dhidi ya wahusika wa mauaji ya raia waliouawa wakati wa maandamano.
Pande hizo mbili pia zilijadili kuhusu uchaguzi wa wabunge sababu kubwa za mgogoro huo.
Hata hivyo upinzani haujatoa majibu yake rasmi, lakini tayari umeonyesha kuwa umeridhika, wakati, kwa upande wa Imam Mahmoud Dicko, mazungumzo bado yanawezekana.
Baada ya kukutana na ujumbe wa ECOWAS nchini Mali, Choguel Maiga, mmoja wa wasemaji wa upinzaji, aamekumbusha mapendekezo ambayo yalitolewa: "Kwanza, Rais wa Jamhuri atabaki."
Kuna pia mazungumzo ya kuteua wajumbe wapya wa Mahakama ya Katiba kumaliza mizozo ya uchaguzi.
Serikali hii ya umoja wa kitaifa itakuwa na jukumu la kufanya mageuzi ya kisiasa. Hata kama upinzani nchini Mali unadai kwamba utatoa majibu yake rasmi kwa mapendekezo yaliyotolewa baada ya mkutano wao usiokuwa wakawaida, tayari baadhi wameonyesha kupinga mapendekezo hayo. "Mapendekezo haya yamepunguza vita yetu yote kwa maswali ya uchaguzi", amebaini Choguel Maïga.