COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Alassane Ouattara aendelea kushinikizwa na chama chake kuwania kiti cha urais

Mkurugenzi mtendaji wa chama tawala cha RHDP nchini Cote d’Ivoire Adama Bictogo amesema rais Allasane Ouattara ndie mgombea pekee anayeweza kupambana na upinzani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwisho wa mwezi Oktoba.

Kulingana na mtu aliye na ukaribu na ofisi ya rais, Alassane Ouattara "bado anasita" kutekeleza ombi la chama chake.
Kulingana na mtu aliye na ukaribu na ofisi ya rais, Alassane Ouattara "bado anasita" kutekeleza ombi la chama chake. John MacDougall/Pool via REUTERS/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inaoneha kuwa huenda rais  Ouattara akatangaza kuwania muhula wa 3, baada ya kutokea kwa kifo cha waziri mkuu Amadou Gon Coulibaly hivi karibuni ambaye alikuwa mrithi wake.

Hata hivyo hakuna uthibitisho rasmi wakati huu kukiwa na taarifa kwamba rais Ouattara bado anasita kuchukuwa maamuzi, huku waziri wa ulinzi wa sasa Hmaed Bakayoko anaetarajiwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu huenda akateuliwa kuwania nafasi ya urais.

Ingawa bado hajatangaza rasmi nia yake, Alassane Ouattara sasa amendelea kushinikizwa na chama chake kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa urais ujao.

Miezi michache iliyopita, Rais wa Cote d'Ivoire alisema hatowania katika uchaguzi wa urais ujao na kuachia nafasi kwa kizazi kipya kuliendeleza taifa hilo la Afrika, lakini kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly ambaye alikuwa aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama tawala katika uchaguzi wa urais, kimebadili hali ya mambo.