DRC-MAUAJi-USALAMA

Tano waangamia katika shambulio Ituri

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS

Watu watano wameuwa na wanawake saba kubakwa baada ya waasi wa CODECO kushambulia vijiji vinne katika eneo la Djugu mkoani Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na mauaji na ubakaji, ripoti zinasema kuwa waasi hao waliiba mbuzi kutoka vijiji hivyo pamoja na vitu vingine vya thamani.

Visa hivi vya mashambulizi vimeendelea kushuhudiwa katika mkoa wa Ituri na kusababisha raia kuishi kwa wasiwasi huku wengine yakilazilika kuyakimbia makwao.

Hivi karibuni serikali ya DRC ilianziasha mchakato wa amani katika mkoa huo wa Ituri na kuyataka makundi yenye silaha kuweka silaha chini na kuweza kujiunga katika mchakato huo.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi alituma ujumbe wa waliokuwa waasi wa zamani jimboni Ituri miongoni mwao kiongozi wa Kundi la wapiganaji wa FNI Floribert Njabu, kuwahamasisha wapiganaji wa CODECO kukubali kuweka silaha chini,na kuacha kuuwa watu huko Djugu, mkoani Ituri, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Wiki mbili zilizopita kundi la wapiganaji la Nduma Defense of Congo-Rénové (NDC-R) linaloendesha harakati zake Mashariki mwa DRC lilitangaza kwamba limemvua mamlaka ya uongozi kiongozi wake Guidon Shimiray, akishtmiwa "tabia ya kupotoka" kinyume na mapambano ya kundi hilo, "ukiukwaji mkubwa wa sheria za kibinadamu za kimataifa na haki za binadamu"

Naibu kiongozi wa kundi hilo, alisema yuko tayari kuweka chini silaha na kumuunga mkono Félix Tshisekedi katika mchakato wa amani.

Mapema mwezi huu wa Julai Ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (UNJHRO) iliripoti kuongezeka kwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika Mkoa wa Ituri.