MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Upinzani nchini Mali wafutilia mbali mapendekezo ya ECOWAS

Upinzani nchini Mali umetupilia mbali mapendekezo yaliotolewa na ujumbe wa ECOWAS uliohitimisha ziara yake nchini humo baada ya kukutana na pande mbalimbali kujaribu kusuluhisha mzozo wa kisiasa unaoshuhudiwa katika taifa hilo, ambao umesababisha maandamano hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu 11.

Juni 5, makumi ya maelfu ya watu walikusanyika katika mji wa Bamako, mji mkuu wa Mali, wakiomba Rais Ibrahim Boubacar Keita kujiuzulu.
Juni 5, makumi ya maelfu ya watu walikusanyika katika mji wa Bamako, mji mkuu wa Mali, wakiomba Rais Ibrahim Boubacar Keita kujiuzulu. MICHELE CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa ECOWAS umekamilisha shughuli zake nchini Mali, lakini hata hivyo mpango uliowasilishwa na wataalam wa Jumuiya hiyo ya nchi za Afrika Magharibi haukukubaliwa na upinzani, ambao ulitaka kujiuzulu kwa Rais Ibrahim Bubakar Keita.

Wataalam hao wa ECOWAS wamebaini kwamba matatizo ya nchini Mali yanahusishwa na matatizo ya utawala na hivyo wamependekeza mambo matatu.

La kwanza ni uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa na utatuzi wa mizozo ya uchaguzi, na makubaliano ya Mahakama ya Kikatiba ili kwamba Mawaziri waweze kutawala tena juu ya matokeo ya uchaguzi uliopita wa wabunge.

Pendekezo la pili kutoka kwa wataalam wa ECOWAS ni uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa. Ujumbe huo haupendekezi kuondoka kwa Waziri Mkuu, lakini idadi ya wizara kwa kila chama: 50% kwa chama madarakani, 30% kwa upinzani na 20% kutoka kwa mashirika ya kiraia.

Tume ya ECOWAS pia inapendekeza kuanzishwa kwa uchunguzi ili kubaini ni nani anayehusika na kuwafyatulia risasi waandamanaji na uharibifu wa majengo ya umma wakati wa maandamano.