Mgogoro wa kisiasa nchini Mali: Marais wanne wa Afrika wasubiriwa katika ziara yao nchini Mali
Marais wanne wa nchi za Afrika Magharibi wanatarajia kufanya ziara Alhamisi hii, Julai 22 huko Bamako kwa lengo la kusuluhisha mzozo wa kisiasa kati ya vuguvugu la M5 na Rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita (IBK).
Imechapishwa:
Haijafahamika ikiwa hii ni hatua ya mwisho katika kusuluhisha mgogoro huo unaoendelea nchini Mali, baada ya ujumbe wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi uliokuwa ukiongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan kushingwa kusuluhisha pande mbili zinazokinzana nchini Mali, wiki iliyopita.
Upinzani nchini Mali ulitupilia mbali mapendekezo yaliotolewa na ujumbe wa ECOWAS uliohitimisha ziara yake nchini humo baada ya kukutana na pande mbalimbali kujaribu kusuluhisha mzozo wa kisiasa unaoshuhudiwa katika taifa hilo, ambao ulisababisha maandamano hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu 11.
Ujumbe huu wa ngazi ya juu wa ECOWAS unaoundwa na Rais wa Nigeria Mahamadou Issoufou, Rais wa Senegal Macky Sall, Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo na Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara, unatarajiwa mjini Bamako Alhamisi wiki hii. Wengi wanajiuliza iwapo watakuja na mapendekezo mapya, kinyume na yale yaliyotolewa na ujumbe wa hivi karibuni wa jumuiya hiyo.
Wataalam wa ECOWAS walibaini kwamba matatizo ya nchini Mali yanahusishwa na matatizo ya utawala na hivyo walipendekeza mambo matatu.
La kwanza ni uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa na utatuzi wa mizozo ya uchaguzi, na makubaliano ya Mahakama ya Kikatiba ili kwamba Mawaziri waweze kutawala tena juu ya matokeo ya uchaguzi uliopita wa wabunge.
Pendekezo la pili kutoka kwa wataalam wa ECOWAS ni uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa. Ujumbe huo haupendekezi kuondoka kwa Waziri Mkuu, lakini idadi ya wizara kwa kila chama: 50% kwa chama madarakani, 30% kwa upinzani na 20% kutoka kwa mashirika ya kiraia.
Hata hivyo upinzani ulifutilia mbali mapendekezo hayo na kuendelea kudai rais wa nchi hiyo IBK na serikali yake wajiuzulu.