DRC-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus nchini DRC: Rais Tshisekedi atangaza kuondoa hali ya dharura ya kiafya

Zoezi la kunyunyuzia dawa majengo ya serikali katikaWilaya ya Gombe huko Kinshasa katiika kupambana na janga la Corona (picha kumbukumbu).
Zoezi la kunyunyuzia dawa majengo ya serikali katikaWilaya ya Gombe huko Kinshasa katiika kupambana na janga la Corona (picha kumbukumbu). AFP/Junior Kannah

Katika hotuba yake kwenye redio na runinga ya taifa, Rais Tshisekedi ametangaza kumalizika kwa hali ya dharura ya kiafya Jumanne jioni, Julai 21 saa sita usiku. Lakini shughuli za kawaida zitaanza ten ahatua kwa hatua.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia Julai 22, shughuli zote za kibiashara zinaweza kuanza tena rasmi: maduka, mabenki, mikahawa, vilabu, makampuni, hata kama, baadhi shughuli zilikuwa zilianza tena nchini humo.

Felix Tshisekedi pia alizungumzia juu ya kuanza tena kwa mikusanyiko ya watu, mikutano na sherehe. Kufikia sasa, mikusanyiko ya watu zaidi ya 20 imekatazwa. Pia, ametangaza kuanza tena kwa usafiri wa umma leo Jumatano.

Shule na Vyuo Vikuu vimepangwa kuanza tena Agosti 3. Lakini tarehe muhimu zaidi ya kufunguliwa kwa maeneo ya ibada, sehemu za starehe, viwanja vya mpira, viwanja vya ndege na mipaka ni Agosti 15. Hata hivyo masharti yanayohusiana na mazishi yataendelea kuzingatiwa, amesema Rais wa DRC.

Rais Tshisekedi amebaini kwamba hatu ya kuondoa hali ya dharura ya kiafya imetokana hatua iliyopigwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 ambazo zilipelekea idadi ya vifo kupungua na idadi ya wagonjwa waliopona kuongezeka.

Sababu nyingine, labda muhimu zaidi, rais wa DRC amezungumzia juu ya athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga la Corona ambalo limesababisha mdororo wa kiuchumi nchini DRC.

Hata hivyo, rais Tshisekedi amewataka raia wa nchi hiyo kuendelea kuchukua tahadhari.