COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Wabunge wa chama cha RHDP wamtaka Alassane Ouattara kuwania kiti cha urais

Ikiwa zimesalia siku zaidi ya siku 100 kabla ya uchaguzi wa urais nchini Cote d'Ivoire, rais anayemaliza muda wake nchini humo Alassane Ouattara anaendelea kupata shinikizo la kuwania kwenye kiti cha urais, siku chache baada ya kifo cha waziri mkuu Amadou Gon Coulibaly.

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara, Novemba 2019.
Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara, Novemba 2019. John MacDougall/Pool via REUTERS/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Amadou Gon Coulibaly, ambaye alifariki dunia wiki chache zilizopita ndiye angelipeperusha bendera ya chama tawala cha RHDP katika uchaguzi wa urais nchini cote d'Ivoire.

Kifo cha Amadou Gon Coulibaly kimezua sintofahamu katika chama hicho, huku alassane Ouattara akiendela kupata shinikizo la kupeperusha bendera ya chama hiocho.

Wabunge, maseneta, lakini pia mameyakutoka chama hicho madarakani wanakutana Jumatano na Alhamisi wiki hii kujadili na mtu atakayepeperusha bendera ya chama cha RHDP.

Hata hivyo wabunge kutoka chama hicho tayari wameweka wazi msimamo wao na kumtaka Rais Alassane Ouattara kuwania katika uchaguzi wa urais kwa muhula wa tatu.

Hata hivyo hakuna uthibitisho rasmi wakati huu kukiwa na taarifa kwamba rais Ouattara bado anasita kuchukuwa maamuzi, huku waziri wa ulinzi wa sasa Hmaed Bakayoko anaetarajiwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu huenda akateuliwa kuwania nafasi ya urais.

Ingawa bado hajatangaza rasmi nia yake, Alassane Ouattara sasa amendelea kushinikizwa na chama chake kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa urais ujao.

Miezi michache iliyopita, Rais wa Cote d'Ivoire alisema hatowania katika uchaguzi wa urais ujao na kuachia nafasi kwa kizazi kipya kuliendeleza taifa hilo la Afrika, lakini kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly ambaye alikuwa aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama tawala katika uchaguzi wa urais, kimebadili hali ya mambo.