ECOWAS na marais wa Afrika wana matumaini ya kusuluhisha mgogoro wa Mali
Marais watano wa nchi za Magharibi mwa Afrika wanatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Mali, Bamako kujaribu kutatua mgogoro unaoendelea nchini humo.
Imechapishwa:
Ujumbe huo wa nchi tano unaoongozwa na rais wa sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, Mahamadou Issoufou.
Licha ya ujumbe wa wiki iliyopita nchini Mali, hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya utawala na upinzani.
Alhamisi hii, Julai 23, wakati wananchi wa Mali wanatarajia utatuzi wa mgogoro huo, maelewano yanatakiwa kupatikana na pande zote zitatkiwa kueleweshwa kuhusu mpango wa kisiasa lakini pia wa kitaasisi.
Mbali na mgogoro huo wa kisiasa, kwa sababu Mali haina serikali kwa siku 40 sasa, mvutano wa kitaasisi haujapatiwa ufumbuzi.
Mahakama ya Katiba inaendelea kuzidisha mvutano. Tangu ilipofutilia mbali sehemu ya matokeo ya uchaguzi wa wabunge mwezi Mei 2020, kwa faida ya chama madarakani na washirika wake, kulingana na upinzani, wabunge 31 wameendelea kudai warudishwe kwenye nafasi zao. Hii ni moja ya mapendekezo ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, lakini hadi leo, swali hilo bado halijapatiwa ufumbuzi. Mahakama ya Katiba, iliyofutwa na Rais IBK, bado haijapata wajumbe wapya kufikia sasa.
Marais hao watano kutoka nchi wanachama wa ECOWAS lengo la ziara yao nchini Mali sio kujadili makubaliano mapya. Madhumuni yao ni kujikita kwa kile kilichoandaliwa na ujumbe wa Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi. Suala la kujiuzulu kwa rais wa Mali, madai yanayotolewa na upinzani, halimo kwenye mapendekezo ya ujumbe huo unaoongozwa na rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, ambaye ni rais wa sasa wa ECOWAS.
Kulingana na duru tulio nazo, upinzani haudai tena suala la kujiuzulu kwa rais Ibrahim Boubacar Keita, Lakini unaomba Waziri Mkuu Boubou Cissé, ajiuzulu; "Suala hilo halina mjadala, " amesema mmoja wa wanasiasa wa upinzani.