NIGERIA-USALAMA

Wafanyakazi watano wa mashirika ya kutoa misaada wauawa Nigeria na kundi la wanajihadi

Gari la wanajihadi wa kundi la Iswap, lililotekwa na jeshi la Nigeria wakati wa operesheni dhidi ya ugaidi.
Gari la wanajihadi wa kundi la Iswap, lililotekwa na jeshi la Nigeria wakati wa operesheni dhidi ya ugaidi. AUDU MARTE / AFP

Wafanyakazi watano wa mashirika ya kutoa misaada, raia wa Nigeria, ikiwa ni pamoja na mfanyakazi wa shirika lisilo kuwa la kiserikali, Action Contre la Faim (ACF), raia wa Ufaransa, wameuawa na wanajihadi ambao waliwateka nyara kaskazini mashariki mwa Nigeria. eneo lionalokumbwa na vita dhidi ya Boko Haram.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa kundi la Islamic State huko Afrika Magharibi (Iswap) hapo awali walirusha hewani video inayoonyesha mauaji ya kinyama ya watu hao watano.

"Ni kwa huzuni mkubwa, tunatangazia kifo cha Ishaku Yakubu, mfanyakazi wa shirila llisilo la kiserikali la ACF (Action Contre la Faim), aliye uawa kikatili kwenye eneo la Monguno, na wafanyakazi wengine wanne wa mashirika ya kutoa misaada waliotekwa nyara na kundi la watu wenye silaha, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, katika Jimbo la Borno, Juni 8, 2020, "shirika hilo limetangaza katika taarifa yake.

Wakati huo huo shirika lingine lisilo kuwa la kiserikali la International Rescue Committee (IRC), limethibitisha kwamba mmoja wa wafanyakazi wake pia aliuawa.

"IRC inalaani vikali mauaji ya kinyama ya mfanyakazi mwenzetu, Luka Filibus, na wenzake waliotekwa nyara," IRC imesema. "Tunalaani kitendo hicho cha kinyama na tunaomba mwili wake ukabidhiwe familia yake mara moja."

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, ametoa rambirambi zake "kwa familia za wafanyakazi hao watano wa mashirika ya kutoa misaada" na kuahidi kwamba wanajihadi "wataangamizwa kabisa".