DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

Kesi ya Vital Kamerhe yaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa, Kinshasa

Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa.
Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa. AFP PHOTO/ ADIA TSHIPUKU

Mahakama ya Rufaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasikiliza leo Ijumaa kesi ya Vital Kamerhe, Mkurugenzi mkuu katika ofisi ya rais Felix Tshisekedi, na mshirika wake mkuu wa serikali.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya mwanzo ilimuhukumu Vital Kamerhe kifungo cha miaka 20 kwa ufisadi na wizi wa takriban dola za Marekani milioni 50.

Bw. Kamerhe ni mwanasiasa maarufu katika siasa za taifa la DR Congo na ndie mtu muhimu wa muungano uliomsaidia rais Felix Tshisekedi kushinda uchaguzi na kuchukua madaraka.

Alimuunga mkono Tshisekedi katika kampeni zake za mwaka 2018 akitarajia kwamba atarejesha mkono mwaka 2023.

Vital Kamerhe ndie mwansiasa mkuu zaidi kukabiliwa na mashtaka katika taifa hilo kubwa la Afrika ya Kati ambapo kuna ufisadi wa kiwango cha juu.

Kamerhe alikana kuiba fedha zilizotengewa mradi wa ujenzi wa nyumba za serikali chini ya uogozi wa rais Tshisekedi na kuyataja mashtaka hayo kuwa ya kisiasa.

Wakili wake Jean Marie Kabengela Ilunga aliutaja uamuzi huo wa mahakamaya mwanzo kama ukiukaji wa haki za kibinadamu na kusema kwamba atakata rufaa.