MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mkutano wa ECOWAS kuhusu mgogoro wa Mali kufanyika wiki ijayo

Mkutano wa dharura wa nchi za Jumuiya ya Afrika magharibi ECOWAS, unatarajiwa kufanyika Jumatatu wiki ijayo kwa njia ya video ambapo hatua kadhaa zinazoambatana na usuluhishi wa mzozo wa Mali zitachukuliwa.

Viongozi wa ECOWAS nchini Mali.
Viongozi wa ECOWAS nchini Mali. Facebook/Femi Adesina
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja baada ya marais watano kutoka nchi za ECOWAS kukutana Alhamisi wiki hii na wadau mbalimbali wakiwemo rais Ibrahim Boubakar Keita, wawakilishi wa upinzani na mashirika ya kiraia kujaribu kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Mali, huku kinara wa Upinzani Imam Mahamoud Dicko akisema hakuna hatua chanya yoyote imefikiwa na kwamba watu waliopoteza maisha hawawezi kufia bure.

Rais wa Niger Mahamadou Issoufou ndiye mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS .

Madai ya upinzani ni kuona rais Ibrahim Boubakar Keita anajiuzulu, jambo ambalo ECOWAS inasema ni kinyume na demokrasia.