Sudani: Miili 28 ya maafisa wa jeshi yagunduliwa Omdurman
Imechapishwa:
Miili ya maafisa 28 wa jeshi la Sudan, waliohusika katika mapinduzi ya 1990 yaliyotibuliwa dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo Omar al-Bashir, imegunduliwa kwenye kaburi la halaiki katika wilaya ya Omdurman, karibu na Khartoum amesema mwendesha mashtaka wa jamhuri.
Mapema wiki hii kesi mpya inayomkabili aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir ilianza. Omar al-Bashir aliondoka madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Aprili 2019.
Mapinduzi ya Omar El Bashir yalifanyika mwaka 1989 dhidi ya Sadiq al-Mahdi, Waziri Mkuu wa wakati huo wa Sudan na kushika hatamu za uongozi wa nchi.
Anatuhumiwa kukiuka agizo la katiba na anakabiliwa na adhabu ya kifo. Omar al-Bashir atahukumiwa na watu wengine 16, raia wa kawaida na askari, akiwemo Makamu wa Rais Taha na Jenerali Bakri Hassan Saleh.