ZAMBIA-CORONA-AFYA

Wabunge 15 wa Zambia waambukizwa virusi vya Corona

Wabunge 15 wa Zambia wamekutwa na virusi vya Corona baada ya zoezi la lazima la upimaji wa virusi vya corona katika bunge la nchi hiyo, amesema Waziri wa Afya wa Zambia Chitalu Chilufya.

Moja ya Hopitali kuu za mji wa Lusaka,  Zambia.
Moja ya Hopitali kuu za mji wa Lusaka, Zambia. DAWOOD SALIM / AFP
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo la upimaji kwa wabunge wa nchi hiyo liliamrishwa baada ya wabunge wawili kufariki dunia juma lililopita.

Kufikia sasa Zambia ina visa 3,856 vya maambukizi ya virusi vya Corona, na vifo 136 vilivyotokana na ugonjwa huo hatari, huku wagonjwa 1,941 wakithibitishwa kupona.

Ugonjwa huo ambao ulianzia katika mji wa Wuhan nchini China umesababisha vifo 638,000 duniani baada ya vipo vipya 7,096 kuthibitishwa.

Hivi karibuni Shirika la Afya Dunia, WHO, lilionya kutokana na kuchelea kuanza kwa mripuko huo barani Afrika visa vyake katika kipindi hiki vinaongezeka kwa kasi.