SOMALIA-EU-SIASA-USALAMA

EU yaghadhabiswa na hatua ya kumfuta kazi Waziri Mkuu wa Somalia

Mkuu sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell.
Mkuu sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell. REUTERS/Francois Lenoir

Kulingana na mkuu sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, ambaye amezungumza kupitia ujumbe uliochapishwa na idara ya mambo ya nje ya umoja huo, kuachishwa kazi kwa Waziri Mkuu ni utaratibu ulio kinyume na katiba.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya unabaini kwamba hatua hiyo ya Bunge la Somalia inaweza inakwenda kinyume kabisa na ahadi zilizofikiwa na washirika wake wa kimataifa kwa kujumuishwa kwa majimbo ya shirikisho na kushirikishwa na serikali ya Mogadishu kwa minajili ya kudumisha maani nchini Somalia.

Umoja Ulaya umelaani kufukuzwa kwa Waziri Mkuu wa Somalia, Hassan Ali Khaire. Kulingana na Josep Borrell, "Somalia bado ina njia ndefu kwa kupata amani na usalama, kwa kujitoa katika mzigo wa madeni nakuwa huru kwa kuwachaguwa viongozi wake wa kisiasa."

Josep Borrell ametoa wito kwa viongoziambao umetumwa kwa rais Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo na kwa wabunge waliopiga kura ya kumfuta kazi Waziri Mkuu.

Kwa upande wa Ulaya umesema kura hiyo haiendani na misingi ya katiba ya Somalia, ambayo Umoja aw Ulaya unaunga mkono kifedha. Josep Borrell anasema Ulaya inainyooshea kidole cha lawama serikali ya Mogadishu kuhusika na hali hiyo.