DRC-SIASA-USALAMA

Hali ya wasiwasi yatanda Kipupu, DRC

Askari wa Jeshi la DRC, FARDC.
Askari wa Jeshi la DRC, FARDC. REUTERS/Kenny Katombe

Hali ya wasiwasi inaedelea kutanda katika kijiji cha Kipupu siku kumi baada ya mauaji ya watu wasiojulikana idadi katika milima ya mkoa wa Mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitekelezwa na kundi la watu wenye silaha. Hivi karibuni kundi la wanamgambo wa Twirwaneho, walidai kuhusika na shambulio hilo. Lakini idadi ya vifo na haijajulikana mpaka sasa kutokana na kuwa si rahisi kufika eneo la tukio.

Kwa karibu mwaka mmoja sasa, machafuko yameendelea kuongezeka katika eneo hilo. Hata hivyo shambulio hilo limeendelea kuzua hisia tofauti, hasa katika mitandao ya kijamii.

Kwenye kurasa wake wa Twitter, Daktari Mukwege na mshindi wa tuzo ya Nobel amelaani "mauaji ya kikatili katika kijiji cha Kipupu, sambamba na mauaji yanayoendelea kuikumba DRC tangu mwaka 1996" na vita vya kwanza vya Kongo

Mpaka sasa, habari juu ya shambulio lililotokea katika kijiji cha Kipupu usiku wa Julai 16 kuamkia 17 bado zinaleta utata kuhusu idadi ya watu waliouawa.

Kulingana na watafiti kutoka kitengo cha usalama cha KST, wakinukuu mtandao wa vyanzo kutoka eneo hilo, raia 18 waliuawa. Lakini katika taarifa, wabunge wa mkoa wa Kivu Kusini wamebaini kwamba "watu zaidi ya 220 waliuawa, wanawake walibakwa, nyumba zilichomwa moto na mifugo iliyoibiwa".

Akihojiwa na RFI, msemaji wa jeshi la DRC amebaini kwamba jeshi wala tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO hawakuwepo wakati wa shambulio hilo. Kwa hivyo ni ngumu kujua hali hali.

Tangu wakati huo, FARDC inadai kwamba inalinda eneo hilo. Ujumbe wa wabunge wa mkoa na timu ya MONUSCO wanatarajia leo Jumatatu kuzuru eneo la shambulio, kujaribu kupata ukweli zaidi.