DRC-UCHUMI

Sarafu ya DRC, Faranga, yapoteza thamani

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wananchi wa taifa hilo kubwa Afrika ya Kati wameghadhabishwa na jinsi sarafu yao, Faranga ya Congo, ambayo inaendelea kupoteza thamani yake dhidi ya dola ya Marekani.

Faranga za Congo (picha ya kumbukumbu).
Faranga za Congo (picha ya kumbukumbu). Capture d'écran du site du ministère congolais de RDC.
Matangazo ya kibiashara

Kwa kipindi tu cha miaka mitano, sarafu ya DRC, Faranga ya Congo imepoteza zaidi ya 50% ya thamani yake. Hivi leo, dola moja ya Marekani inauzwa zaidi ya faranga 2000 za Congo.

Hayo yanajiri wakati uchumi nchini humo unaendeleakudorora kutokana na janga la Corona huku kitisho cha mfumko wa bei kikiendelea kuwatia wasiwasi wananchi wa taifa hilo, lenye utajiri wa maliasili.

Raia wanasema mfumko wa bei unaweza kuathiri zaidi uchumi wa taifa hilo.

"Inabidi sasa tuanze kubana matumizi.Tunapaswa kupunguza matumizi ya kila siku," anasema. Na kile ambacho watoto walikuwa wakipata baada ya chakula, kama vile matunda, hawapati tena kwa sababu tunajikita tu kuwa na chakula cha jioni na kifungua kinywa asubuhi, " amesema Évan, mama wa familia ,a na mfanyakazi wa serikali.

"Ni mateso yanayoongezeka, amebaini Lemien Saka, huku akiongza kuwa watu wote sasa wanakabiliwa na hali ngumu na kwa sasa wamekata tamaa kutokana na hali ngumu ya maisha.

Hakuna kinachofanyika ili kuepo na mabadiliko. Unapouliza kuhusu hali hiyo, jibu linakuja ni kuwa ni kutokana na janga la Corona, ni masikitiko makubwa, amesema Lemien Saka.

Hivi karibuni rais Félix Tshisekedi aliwaagiza Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki kuu kuchukuwa hatua madhubuti ili sarafu ya Congo, Faranga ya Congo, isiendelei kupoteza thamani yake.

Wakati huo huo mashirika ya kiraia yanabaini kwamba tangu kuwasili kwa Tshisekedi madarakani, maisha yamekuwa magumu na mapato yanaendelea kupungua.