SOMALIA-MAREKANI-USALAMA

Somalia: Jeshi la Marekani lakiri kutokea vifo vya raia katika mashambulizi yake ya anga

Ndege ya kijeshi ya mizigo ya Marekani nchini Somalia, mwaka 2017 (picha ya kumbukumbu).
Ndege ya kijeshi ya mizigo ya Marekani nchini Somalia, mwaka 2017 (picha ya kumbukumbu). US Air Force

Marekani imekir kwamba mashambulizi yake ya anga nchini Somalia yamesababisha vifo vya raia wa kawaida, Hili ni tukio lisilo kuwa la kawaida Marekani kukubali kutokea kwa vifo vya raia katika mashambulizi yake nchini Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ya makao makuu ya jeshi la Marekani barani Afrika, Africom, Mashambulizi yaliyotekelezwa Februari 2 yalisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu.

Wanaharakati wa haki za binadamu wamekaribisha hatua hiyo ya jeshi la Marekani kukiri makosa katika operesheni yake ya kijeshi nchini Somalia.

Hii ni mara ya tatu kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi Washington kukiri vifo vya raia nchini Somalia. Taarifa ambayo imechapishwa katika ripoti ya baada ya miezi mitatu ya Africom kuhusu mashambulizi yake ya anga nchini Somalia.

Februari 2, bomu lililorushwa dhidi ya watu walioshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu wa Al-Shabab katika mkoa wa Jilib, Kusini mwa Mogadishu, liliua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu. Kulingana na shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International, mtu huyo aliyeuawa alikuwa mwanamke na watu watatu kutoka familia yake, ambao hawakuwa na uhusiano wowote na magaidi hao.

Chunguzi nne bado zinaendelea

"Lengo letu ni kupunguza athari kwa raia. Kwa bahati mbaya, hatukuwa tunawalenga watu hawa, "Jenerali Stephen Townsend, kamanda wa wa Marekani barani Afrika.

Uchunguzi wa ishirini na saba kuhusu matukio kama hayo yamekamilishwa na chunguzi nne bado zinaendelea, makao makuu ya jeshi la Marekani barani Afrika yamesema.