ZIMBABWE-UN-USALAMA-CORONA-UCHUMI

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu baa la njaa Zimbabwe

Umoja wa mataifa umeonya kuwa huenda asilimia sitini ya watu nchini wa Zimbabawe wakakabiliwa na baa la njaa kutokana na athari za virusi vya Corona wakati huu shirika la  mpango wa chakula, WFP, likiomba msaada wa Dola millioni 250 kukabiliana na hali hiyo.

Polisi ikipiga doria wakati raia wakiendelea kuzuiliwa kutembea kwa hofu ya kuambukizwa virusi vya Corona, Harare, Zimbabwe, Aprili 3, 2020.
Polisi ikipiga doria wakati raia wakiendelea kuzuiliwa kutembea kwa hofu ya kuambukizwa virusi vya Corona, Harare, Zimbabwe, Aprili 3, 2020. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Shirika  la Mpango wa  Chakula duniani, WFP, linasema kuwa idadi ya watu watakaokabiliwa na baa hilo la njaa iwapo msaada hautakuja kwa wakati, itafikia zaidi ya Milioni Nane kufikia mwezi Desemba.

Aidha, WFP inasema idadi ya watu watakaopoteza ajira nchini humo itaongezeka kutokana na makataa ya watu kutotoka nje kutokana na janga la Corona.

Hivi karibuni, imeripotiwa idadi kubwa ya watu wanaorudi vijiji kutoka mijini kwa hofu ya janga la Corona, hali ambayo inaendelea kutia hofu.

Katika hatua nyingine, maandamano ya wapinzani yanatarajiwa kushuhudiwa nchini humo siku ya Ijumaa, kulalamikia hali ngumu ya kiuchumi na madai ya ufisadi katika serikali ya rais Emmerson Mnangagwa.

Serikali tayari imetuma maafisa wa polisi katika maeneo mbalimbali nchini humo kabiliana na waandamanji hao.