DRC-KISANGANI-SIASA-UCHUMI

DRC: Wakazi wa Tshopo wamuomba Gavana Wale Lufungula kujiuzulu

Gavana wa Tshopo Jean-Marie Wale Lufungula, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wakazi wa mkoa huo ambao wanamuomba ajiuzulu haraka iwezekanavyo.

Moja ya mitaa ya katikati mwa jiji la Kisangani (picha ya kumbukumbu).
Moja ya mitaa ya katikati mwa jiji la Kisangani (picha ya kumbukumbu). CC/Creative Commons / Piet Clement
Matangazo ya kibiashara

Mbali na maandamano yaliyozimwa na vikosi vya usalama Jumanne huko Kisangani, mji mkuu wa mkoa wa Tshopo, kundi la wabunge wa mkoa tayari wamemtuhumu kiongozi huyo.

Wabunge kumi na nane kati ya ishirini na nane wanaounda bunge la mkoawa Tshopo wamewasilisha mashtaka dhidi ya Gavana Jean-Marie Wale Lufungula. Na wakazi wa mji wa Kisangani wameamua kuunga mkono hatua hii ya wabunge kwa maandamano kupitia operesheni "Tshopo Telema", kwa maneno mengine "Simama Tshopo".

Kwa upande wa waandamanaji wanasema, Jean-Marie Wale Lufungula anapaswa kujiuzulu kwenye wadhifa wake. Gavana Jean-Marie Wale Lufungula amepewa saa 24 awe amejiuzulu.

Kulingana na muungano wa mashirika ya kiraia, saa 24 ni muda unaoruhusiwa na sheria pale gavana anaposhtakiwa.

Wabunge wa mkoa wa Tshopo wanamshtumu gavana Jean-Marie Wale Lufungula kwa matumizi mabaya naya fedha zilizotengwa kwa kupambana dhidi ya Covid-19 na shughuli za mpango wa siku 100 ulioanzishwa na rais Felix Tshisekedi.

Mbele ya bunge la mkoa, Gavan Jean-Marie Wale Lufungula hakuweza kufafanua kuhusu matumizi ya dola milioni 2.5 za mkopo wa benki ta FNBank, amesema Mateus Kanga, kiongozi wa vuguvugu la Parlement Debout.