LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Uwepo wa mamluki kutoka nchi za kigeni watia wasiwasi Libya

Mamluki wa kigeni wanasaidia vikosi vya jeshi la serikali ya umoja wa kitaifa (GNA). Hapa ni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli, Juni 3, 2020 (picha ya kumbukumbu).
Mamluki wa kigeni wanasaidia vikosi vya jeshi la serikali ya umoja wa kitaifa (GNA). Hapa ni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli, Juni 3, 2020 (picha ya kumbukumbu). AFP

Majirani wa Libya watiwa wasiwasi na uwepo wa maelfu ya mamluki nchini humo. Kwa miezi kadhaa, mamluki kutoka nchi kadhaa wamekuwa wakiingia nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wanabaini kwamba mamluki hao ni wengi mno;, hali ambayo nchi jirani zinasema zinatiwa wasiwasi na uwepo wao nchini Libya.

Mamluki hao wanakadiriwa kufikia 17,000, kulingana na sensa ya hivi karibuni ya shirika la Haki za Binadamu nchini Syria, OSDH. Kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inabaini kwamba mamluki kati ya 12,000 na 15,000 kutoka nchi za kigeni wapo nchini Libya. Wanaisadia vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na Fayez el-Sarraj.

Wengi wa mamluki hao ni kutoka Syria, lakini pia wengine ni kutoka mataifa mengine yaliyohusika katika vita vya jihadi nchini Syria na Iraq. Wengine ni kutoka Tunisia, Algeria, Yemen na Somalia, ambao wote waliingia hivi karibuni katika mji wa Tripoli.

Vyanzo kadhaa vya Libya vinasema kwamba mamluki hawa wanaongozwa maafisa wa idara ya ujasusi na wanajeshi 3,000 wa Kituruki, waliopo nchini Libya kusaidia serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNA). Ankara inataka kwa hali na mali kudhibiti Sirte, mji wa kimkakati, sawa na mji wa Al Joufra. Lakini miji hiyo miwili ni mistari nyekundu kwa Misri ambayo imetishia kuingilia kati.