MALI-SIASA-USALAMA

Waziri Mkuu wa Mali afautilia mbali madai ya upinzani ya kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Mali,Boubou Cissé.
Waziri Mkuu wa Mali,Boubou Cissé. MARCO LONGARI / AFP

Waziri Mkuu wa Mali,Boubou Cissé,amekataa pendekezo la upinzani la kutaka aachie ngazi na kubaini kwamba 'mzozo wa nchi Mali utapatiwa suluhisho kupitia mazungumzo.'

Matangazo ya kibiashara

Wiki hii Waziri Mkuu wa Mali Boubou Cissé alitolea wito upinzani kushiriki katika mazungumzo kwa minajili ya kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Muungano wa kundi la  vuguvu la M5-RFP umeitisha hatua nyingine zaidi za wananchi kutotii sheria za nchi.

Wakati huo huo wabunge 31 ambao Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ilipendekeza wajiuzulu, kupitia kiongozi wao Gougan Coulibaly, wamesema kwamba hawatajiuzulu kwa kuwa pendekezo hilo la ECOWAS linakwenda kinyume na katiba ya Mali.

Mali kwa sasa ina serikali yenye mawaziri sita. Keita ambaye tangu mwezi Aprili alikuwa hana baraza la mawaziri, aliliunda baraza hilo chini ya shinikizo la Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ambayo imehusika katika juhudi za kutanzua mzozo wa nchi yake.