ZIMBABWE-UFISADI-UCHUMI-CORONA

Zimbabwe kukumbwa na maandamano makubwa

Upinzani umeitisha maandamano leo Ijumaawakati serikali ya Zimbabwe imeonya kwamba haitokubali maandamano yoyote kufanyika (picha ya kumbukumbu)
Upinzani umeitisha maandamano leo Ijumaawakati serikali ya Zimbabwe imeonya kwamba haitokubali maandamano yoyote kufanyika (picha ya kumbukumbu) REUTERS/Mike Hutchings

Hali ya sintofahamu inaendelea nchini Zimbabwe, baada ya upinzani kuitisha maandamano hii leo Ijumaa kupinga kashfa ya ufisadi inayoripotiwa katika serikali.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo imeonya kuwa haitavumilia mikusanyiko ya aina yoyote.

Wakati huo huo mamlaka imeweka sheria ya kutotoka nje na kupiga marufuku mikutano yote ya watu zaidi ya 50, kama sehemu ya hatua kudhibiti maambukizi ya virusi vay Corona.

"Hakuna maandamano yatakayofanyika! Msemaji wa polisi wa Zimbabwe alionya jana Alhamisi alasiri. "Vikosi vya usalama viko tayari kukabiliana na yeyote yule atakayeingia mtaani," ameongeza. Siku ya Alhamisi, shughuli nyingi zilizorota, huku maduka kadhaa ya mjini Harare yakifungwa, na vikosi vya usalama vikionekana katika maeneo muhimu ya mji huo.

Upinzani umesema uko tayari kuingia mitaani kupinga ufisadi unaoripitiwa katika serikali.

Wakati huo huo kesi ya Waziri wa zamani wa Afya, aliyetimuliwa wiki 3 zilizopita, akituhumiwa kutumia vibaya pesa zilizotengwa katika mpango wa mapambano dhidi ya Covid-19.

Mwanzoni mwa maandamano hayo, chama kidogo cha upinzani "Transform Zimbabwe" ambacho kiongozi wake Jacob Ngarivhumé alikamatwa na kushtakiwa kwa kufanya vurugu, yeye na mwandishi wa habari Hopewell Chin , baada ya kulalamikia kashfa ambayo Waziri wa zamani wa Afya alihusishwa.

Waandaaji wa maandamano hayo wamewataka wafuasi wao kutovaa sare za vyama vya siasa, wakikumbusha kuwa ni maandamano ya kupinga ufisadi.