ZIMBABWE-UFISADI-UCHUMI-CORONA

Zimbabwe yaendelea kulaumiwa kushindwa kukomesha ufisadi

Polisi na wanajeshi wamekuwa wakipiga kambi katika barabara na mitaa mbambali jijini Harare, baada ya serikali kupiga marufuku maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo kulalamikia kushindwa kudhibiti janga la Corona na madai ya ufisadi katika serikali.

Polisi ya zimababwe imewataka raia wa taifa hilo kutoshiriki katika maandamano ambayo yalikuwa yamepangwa siku ambayo rais Mnangangawa anaadhimisha miaka miwili tangu alipoingia madarakani.
Polisi ya zimababwe imewataka raia wa taifa hilo kutoshiriki katika maandamano ambayo yalikuwa yamepangwa siku ambayo rais Mnangangawa anaadhimisha miaka miwili tangu alipoingia madarakani. Jekesai NJIKIZANA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalikuwa yamepangwa na mwanasiasa wa upinzani Jacob Ngarivhume anayeongoza chama cha Transform Zimbabwe, kulalamikia kuendelea kuyumba kwa uchumi wa taifa hilo na madai ya ufisadi katika serikali ya rais Emmerson Mnangagwa.

Vizuizi viliwekwa barabara kuu katika jiji hilo, huku maafisa wa usalama wakiwataka raia wa taifa hilo kutoshiriki katika maandamano hayo ambayo yalikuwa yamepangwa siku ambayo rais Mnangangawa anaadhimisha miaka miwili tangu alipoingia madarakani.

Kuhofia kutokea kwa vurugu, idadi kubwa ya maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia walionekana mbele ya bunge huku maduka, vitu vya kuuza mafuta na Benki zikifungwa.

Wakati huo huo mwandishi maarufu duniani Tsitsi Dangarembga amekamatwa wakati akiadamana mwenyewe.

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za Binadamu, imeitaka serikali ya Zimbabwe kuacha kutumia virusi vya Corona kama sababu ya kuzuia haki za watu kujieleza na kuandamana.