MALI-TOGO-CHAD-USAFIRI-CORONA

Nchi kadhaa za Afrika Magharibi zafungua tena mipaka yao ya anga

Wasafiri wanaabiri ndege inayofanya safari kati ya  Lagos na Abuja, Nigeria, Julai 9, 2020.
Wasafiri wanaabiri ndege inayofanya safari kati ya Lagos na Abuja, Nigeria, Julai 9, 2020. AP Photo/Sunday Alamba

Baada ya kufungwa kwa miezi mitano kwa sababu ya Covid-19, ndege zinaweza tena kufanya safari katika nchi nyingi za Afrika Magharibi kuanzia leo Jumamosi hii, Agosti 1, kwa masharti kuwa abiria wawe wamefanya vipimo vya PCR na kukutwa hawana virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Tangu katikati mwa mwezi Machi, ndege chache zimeweza kufanya safari kwenda katika eneo la Sahel ya Kati, ikiwa ni pamoja na ndege kadhaa za mizigo, ndege za kijeshi na ndege zilizotumiwa kuwarudisha nyumbani wakimbizi.

Kufikia Jumamosi hii, Agosti 1, safari za ndege katika eneo hilo zinatarajia kuanza, kwani Chad, Niger na Burkina Faso zimefungua tena mipaka ya anga.

Kwa hivyo ndege za kibiashara zitaweza kuanza tena safari, kwa masharti tu wasafiri wote waonyesha cheti cha vipimo na kudhihirika kuwa hawana virusi vya Covid-19 kwa muda wa saa 72.

Hayo yanajiri wakati Shirika la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa kuanza kuondoa masharti ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona katika mataifa mbalimbali barani Afrika, huenda hatua hiyo isababisha maambukizi mapya.

Mwakilishi wa WHO barani Afrika Daktari Matshidiso Moeti ameyatak mataifa ya Afrika pamoja na kuanza kulegeza masharti hayo, kukumbuka kuwa hakuna taifa lililo salama na kuendelea kuwatafuta na kuwapima watu ambao huenda wameambukizwa, kauli inayoungwa mkono na Daktari John Nkengasong Mkuu kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC.

Bara la Afrika kwa sasa lina maambukizi zaidi ya Laki tisa.