SOMALIA-CORONA-UCHUKUZI

Safari za ndege kurejelewa tena Somalia Agosti 3

Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.
Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. STUART PRICE / AU-UN IST PHOTO / AFP

Serikali ya Somalia kupitia waziri wake wa mawasiliano, Mohamed Maareye, imetangaza kurejelewa kwa safari za ndege za kimataifa kuanzia agosti tatu, huku shule na vyuo vikuu vikifunguliwa agosti 15, baada ya kufungwa kutoka na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mohamed , amesema hilo limeafikiwa baada ya mkutano wa bazara la mawaziri, taifa hilo hadi sasa lina visa 3,212 vya maambukizi ya corona na vifo 93.

Hayo yanajiri wakati Shirika la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa kuanza kuondoa masharti ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona katika mataifa mbalimbali barani Afrika, huenda hatua hiyo isababisha maambukizi mapya.

Mwakilishi wa WHO barani Afrika Daktari Matshidiso Moeti ameyataka mataifa ya Afrika pamoja na kuanza kulegeza masharti hayo, kukumbuka kuwa hakuna taifa lililo salama na kuendelea kuwatafuta na kuwapima watu ambao huenda wameambukizwa, kauli inayoungwa mkono na Daktari John Nkengasong Mkuu kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC.

Bara la Afrika kwa sasa lina maambukizi zaidi ya Laki tisa.