ZIMBABWE-UFISADI-UCHUMI-CORONA

Watu kadhaa wakamatwa baada ya maandamano Zimbabwe

Eneo la katikati la mji mkuu wa Zimbabwe, Harare lilikuwa limezingirwa na maafisa wengi wa polisi kwa lengo la kuzima maandamano yaliyokuwa yliitishwa na upinzani Ijumaa, Julmai 31, 2020.
Eneo la katikati la mji mkuu wa Zimbabwe, Harare lilikuwa limezingirwa na maafisa wengi wa polisi kwa lengo la kuzima maandamano yaliyokuwa yliitishwa na upinzani Ijumaa, Julmai 31, 2020. REUTERS/Philimon Bulawayo

Ijumaa wiki hii kulikuwa kunatarajiwa maandamano makubwa ya upinzani nchini zimbabwe dhidi ya kile wanachodai kuwa ufisadi uliokithiri katika serikali.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wengi wa polisi walionekana katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu Harare, na katika mji wa pili kwa ukubwa wa Bulawayo.

Hata hivyo mikusanyiko ya idadi ndogo ya watu ilionekana katika viunga vya miji hiyo miwili. wakati huo huo watu kadhaa walikamatwa.

Kwa siku za hivi karibuni polisi iliwakamata wanaharakati kadhaa na waandishi wa habari na kuwakabidhi ofisi ya mashitaka ambayo imewafungulia mashitaka. Na hivi sasa wameanza kufikishwa mbele ya mahakama kujibu tuhuma zinazowakabili.

Vizuizi viliwekwa kwenye barabara kuu katika jiji la Harare, huku maafisa wa usalama wakiwataka raia wa taifa hilo kutoshiriki katika maandamano hayo ambayo yalikuwa yamepangwa siku ambayo rais Mnangangawa ameadhimisha miaka miwili tangu alipoingia madarakani.

Hata hivyo maandamano hayo yalikuwa walipigwa marufku na serikali.

Kuhofia kutokea kwa vurugu, idadi kubwa ya maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia walionekana mbele ya bunge huku maduka, vitu vya kuuza mafuta na Benki zikifungwa.

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za Binadamu, imeitaka serikali ya Zimbabwe kuacha kutumia virusi vya Corona kama sababu ya kuzuia haki za watu kujieleza na kuandamana.