DRC-USALAMA

DRC: Kumi na sita wauawa katika mapigano kati ya makundi hasimu Kaseke

Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimamakaribu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmojahuko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018.
Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimamakaribu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmojahuko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018. © AFP

Watu 16 wameuawa na wengine 12 kujeruiwa mwishoni mwa juma lililopita, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya makundi mawili kutoka kundi la waasi la NDC-Renove, katika eneo la Kaseke mkoani Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, mapigano hayo yalizuka baada ya kundi linaloongozwa na Gilbert Bwira kushambulia kijiji cha Kaseke, kinachodhibitiwa na kundi linaloongozwa na Guidon Shirayi Muissa.

Hivi karibuni viongozi katika serikali ya DRC, ukianzia rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi walianzisha mchakato wa kuwasahiwishi waasi kutoka makundi mbalimbali katika Mkoa w Ituri, Kaskazini Mashariki wa DRC, kuweka silaha chini na kujiunga katika mchakato wa amani.

Baadhi ya wapiganaji wameiitikia wito huo, lakini kuna wengine ambao wamepinga na wameapa kuendelea vita dhidi ya utawala wa Tshisekedi.