RCA-SIASA-USALAMA

CAR: Upinzani na mashirika ya kiraia watoa makataa ya siku 3 kwa ajili ya mazungumzo ya kitaifa

Vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Afrika katika ushirikiano na mashirika ya kiraia vimemtaka rais wa nchi hiyo Faustin Archange Touadera kuandaa mazungumzo ya kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu wa urais na ule wa wabunge mwezi Desemba mwaka huu.

Anicet Georges Dologuélé, mgombea urais nchini CAR, akiwasalia wafuasi wake huko Bangui, Desemba 28, 2015.
Anicet Georges Dologuélé, mgombea urais nchini CAR, akiwasalia wafuasi wake huko Bangui, Desemba 28, 2015. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wadau tofauti walimtumia barua rais wa Jamhuri lakini mpaka sasa hajajibu, wamesema. Jumatatu katika mkutano na waandishi wa habari, walitoa wito wa mwisho kabla ya kuchukuwa hatua ambazo wamesema zitakuwa muhimu kwao.

Wito huu wa upinzani unakuja wakati huu nchi hiyo ikishuhudia ongezeko la makundi ya wapiganaji wenye silaha wanaozorotesha usalama wa nchi hiyo.

"Haya sio madai. Ni kumtaka tu rais kuitsha kikao cha mazungumzo na baadhi ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kujadili mchakato huu wa uchaguzi ambao unahusu pande zote, kujadili makubaliano haya ya amani ambayo hayaheshimishwi hata kidogo. Tunaelekea kwenye uchaguzi wakati makundi yenye silaha yanaendelea kudhibiti baadhi ya maeneo, na kusababisha ukosefu wa usalama. [...] Ikiwa rais hajatokea kwa muda wa siku tatu, kwani tayari tumesubiri karibu mwezi mmoja na tunaona kuwa uchaguzi huu kuna hatari ucheleweshwe kutokana na sintofahamu katika maandalizi yake, kwa hiyo tutalazimika kudhihirisha hasira yetu kupitia vitendo kukaidi serikali, " amesema Anicet George Dologuélé ni rais wa chama cha URCA na rais wa muungano wa upinzani COD20-20.