AFRIKA KUSINI-CORONA-AFYA

Rais Ramaphosa aonya maafisa wa serikali wanaofuja fedha za kupambana Corona

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati wa mgogoro wa kafya ykatika kituo cha maonyesho kinachowapokea wagonjwa huko Johannesburg Aprili 24.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati wa mgogoro wa kafya ykatika kituo cha maonyesho kinachowapokea wagonjwa huko Johannesburg Aprili 24. Jerome Delay / POOL / AFP

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa onyo kali dhidi ya watu ambao wamekuwa wakifuja fedha za kupambana na maambukizi ya janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Onyo hili linakuja baada ya ripoti kuwa maofisa wa serikali walikuwa wanajitajirisha kwa kufanya biashara chafu kwenye ununuzi wa vifaa vya kujilinda na chakula cha msaada.

Afrika Kusini ina maambikizi zaidi ya Laki Tano na inakuwa nchi ya kwanza kwa maambukizi hayo barani Afrika.

Hayo yanajiri wakati nchini Gambia, mawaziri watatu wamethibitishWa kuambukizwa virusi vya Corona siku chache baada ya makamu wa rais Isatou Touray kugunduliwa na virusi hivyo .

Rais wa Gambia Adama Barrow ambaye amejitenga kwa siku 14 amesema Waziri wa fedha, Mambureh Njie, ni miongoni mwa mawaziri hao.

Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuwa licha ya kuwepo matumaini makubwa ya chanjo ya virusi vya corona, huenda kusiwe na tiba ya haraka ya ugonjwa wa Covid-19 na kwamba itachukua muda mrefu kabla hali irudi kuwa ya kawaida.

Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amezitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kiafya za kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo kama uvaaji wa barakoa, kuweka umbali wa mtu na mtu, kuosha mikono na kupima virusi hivyo.