DRCHAKI-SIASA

Mpango wa rais Tshesekedi wa kufanya mabadiliko katika mahakama ya Katiba wazua kizaaza

Majaji wa Mahakama ya Katiba ya DRC, Januari 2019.
Majaji wa Mahakama ya Katiba ya DRC, Januari 2019. Caroline THIRION / AFP

Majaji wawili wa mahakama ya kikatiba nchini DRC, Noel Kilomba na Jean Ubulu, wametupilia mbali mpango wa rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi wa kufanya mabadiliko katika mahakama hiyo na kuhamishiwa katika mahakama ya juu.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyoripotiwa katika vyombo vya habari imefahamisha kuwa majaji hao Noel Kilomba na Jean Ubulu kutoka muungano wa wanasiasa unaoungwa mkono na rais wa zamani wa taifa hilo Joseph Kabila, hawakuonekana wakati wa sherehe za kuapishwa kwa mawakili na majaji mbele ya rais Félix Tshisekedi hapo jana siku ya Jumanne.

Mbali na majaji hao, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Spika wa bunge la kitaifa na kiongozi wa Senati pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali, hawakukubali kushiriki kuapishwa kwa majaji hao wapya, kitendo ambacho kimetafsiriwa na upande wa chama cha UDPS kama kupinga maagizo ya rais.

Hata hivyo majaji Noel Kilomba na Jean Ubulu wameelezea msimamo wao kwa rais Félix Tshisekedi katika barua ya Julai 27 ambayo ilizunguka katika mitandao ya kijamii Jumanne wiki hii ambapo idhaa ya kifaransa ya RFI iliipata nakala.

Taarifa zinasema huenda hatua kali za kisheria zikachukuliwa dhidi ya majaji hao ambao inadaiwa kuwa mwenendo wao huenda ukaathiri utendaji kazi katika vyombo vya sheria nchini humo.