MISRI-ETHIOPIA-SUDAN-USHIRIKIANO

Ujenzi wa Bwawa la Renaissance: Misri yajiondoa kwenye mazungumzo na Ethiopia

Bwawa kubwa la Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015.
Bwawa kubwa la Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015. REUTERS/Tiksa Negeri

Serikali ya Misri imetangaza kujiondoa kwenye mazungumzo na Ethiopia kuhusu mzozo wa ujenzi wa bwawa la Renaissance. Hii ni baada ya Ethiopia kuanza mchakato mpya wa kujaza bwawa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Cairo imedai kuwa Ethiopia kwenye mchakato mpya, imeshindwa kuweka bayana taratibu za kujazwa bwawa hilo na namna ya kutatua mizozo.

Ethiopia inasema kukamilika kwa mradi huo mkubwa barani Afrika, ni muhimu sana kwa mustakabili wa taifa hilo na utawaondoa mamilioni ya raia wake kutoka kwenye umasikini na kusambaza umeme barani Afrika.

Hivi karibuni Misri ilitaka kupewa maelezo na serikali ya Ethiopia kuhusu hatua hiyo, ikisema nchi hiyo itategemea asilimia 90 ya maji safi kutoka kwenye mto Nile na mradi huo unatishia uhai wa raia wake.

Mazungumzo ya kimataifa yakiongozwa na Marekani na Umoja wa Mataifa kujaribu kutatua mvutano huu, hayakufua dafu.