COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Wapiga kura wapya Laki Tisa wajiandikisha nchini Cote d'Ivoire

Ikulu ya rais huko Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Côte d’Ivoire.
Ikulu ya rais huko Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Côte d’Ivoire. Présidence de la République de Côte d'Ivoire/Wikimedia/CC 4.0

Tume ya uchaguzi nchini Côte d’Ivoire inasema wapiga kura wapya 900,000 wamejiandikisha katika orodha ya wapigakura kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume hiyo Ibrahime Coulibaly-Kuibiert, ametupilia mbali madai ya upinzani kwamba tume hiyo imekuwa ikiwabagua wapinzani kwa kufuta majina ya baadhi yao katika orodha ya wagombea kiti cha urais nchini humo.

Aidha, amesema mpaka sasa ni wapiga kura milioni 7.5 ndio wamesajiliwa kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Oktoba.

Uchaguzi huo wa Oktoba unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa tangu mwaka 2010 baada ya ushindi wa Ouattara dhidi ya Laurent Gbagbo, ushindi uliochochea vita vilivyosababisha vifo vya watu 3,000.