AFRIKA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yapindukia Milioni moja Afrika

Nusu ya maambukizi ya virusi vya Corona yameripotiwa nchini Afrika Kusini, ambayo kwa sasa watu zaidi ya Laki Tano na Elfu 30 wameambukizwa.
Nusu ya maambukizi ya virusi vya Corona yameripotiwa nchini Afrika Kusini, ambayo kwa sasa watu zaidi ya Laki Tano na Elfu 30 wameambukizwa. REUTERS/Siphiwe Sibeko/File Photo

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona barani Afrika, sasa imefikia zaidi ya Milioni Moja, huku idadi hiyo ikifikia Milioni 19. Idadi ya vifo imepindukia 712,000, huku wagonjwa Milioni 11.5 wakithibitishwa kupona.

Matangazo ya kibiashara

Nusu ya maambukizi hayo yameripotiwa nchini Afrika Kusini, ambayo kwa sasa watu zaidi ya Laki Tano na Elfu 30 wameambukizwa.

Misri, Nigeria na Ghana pia ni mataifa mengine yenye idadi kubwa ya maambukizi, huku idadi ya watu waliopoteza maisha ikifikia 9,604.

Daktari John Nkengasong, Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika, CDC amesema, bara la Afrika lina nafasi ya kushinda janga hili.

Hata hivyo hivi karibu shirika la Afya Duniani, WHO, lilisema linahofia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika, huku likionya kuwa kuendelea kushuhudiwa kwa ongezeko hilo hasa nchini Afrika Kusini, huenda hatua hiyo ikaathiri mataifa mengine barani Afrika.