DRC-ZAMBIA-USALAMA

DRC: Vikosi vya Zambia vyondoka katika maeneo ya Muliro-Kibambe

Barabara kuu huko Kalemi, mkoa wa Tanganyika, DRC, Machi 25, 2016.
Barabara kuu huko Kalemi, mkoa wa Tanganyika, DRC, Machi 25, 2016. RFI/Sonia Rolley

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema vikosi vya nchi jirani ya Zambia vimeondoka katika vijiji viwili huko Muliro-Kibambe katika mkoa wa Tanganyika, baada ya mazungumzo yaliyoongozwa na nchi za SADC.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya miezi minne ya mzozo kati ya Zambia na DRC kuhusu mpaka upande wa eneo la Moba, serkali ya Kinshasa imetangaza kwamba vikosi vya Zambia hatimaye vimeondoka katika ardhi ya DRC.

Hata hivyo kiongozi wa kijiji cha Mulirokilio kwenye mpaka na Zambia huko Moba amebaini kwamba bado kuna vijiji vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vingali mikononi mwa na jeshi la Zambia

Jolino Makelele, waziri wa Habari na msemaji wa sekali ya DRC amesema suluhuu ya mzozo kati ya DRC na Zambia ni matokeo chanya ya mazungmzo yaliyosimamiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, na rais wa Congo Brazzaville Denis Sassou Ngwesso.

Wakaazi wa kijiji cha Kalubamba, moja ya vijiji vilovyovamiwa na jeshi la Zambia tangu mwezi Machi, wanahakikisha kwamba wameanza kurejea makwao, huku wakibaini kwamba wamepoteza mali zao nyingi.

Tangu katikati mwa mwezi Machi, matukio ya mashambulizi yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara kwenye mpaka kati ya DRC na Zambia. Kinshasa inatuhumu jirani yake kwa kutumia ardhi yake na kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini DRC.