LIBYA-IS-USALAMA

Libya: IS yarejea tena katika mji wa Sabratha

Shambulizi la Marekani liliharibu magari ya kundi la IS huko Sabratha, Februari 19, 2016.
Shambulizi la Marekani liliharibu magari ya kundi la IS huko Sabratha, Februari 19, 2016. REUTERS/Sabratha municipality media office/Handout

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wamerejea tena kwa wingi katika mji wa Sabratha, Magharibi mwa Libya. Wapiganaji wa kundi hili walitimuliwa mara kadhaa tangu mwaka 2014 kabla ya kuurejea. Wameendelea kudhibiti baadhi ya maeneo ya mji huo hatu kwa hatua.

Matangazo ya kibiashara

Jiji la Sabratha, kilomita 70 Magharibi mwa mji wa Tripoli, ambao unapatikana karibu na mpaka wa Tunisia, mnamo mwaka 2016 ulikuwa kituo muhimu cha kundi la Islamic State nchini Libya.

Shambulizi la Marekani lililolenga kambi ya mafunzo ya IS karibu na mji huo,na liliua wapiganaji zaidi ya 50 wa kundi hilo, wengi wao kutoka Tunisia.

Kwa mujibu wa mashahidi ambao ni wakaazi wa mji huo, kwa sasa wapiganaji wa IS wanatembea hadharani mchana kweupe huko Sabratha. Wamepiga kambi tena katika kambi mbili (Al Tlil na Al Baraem) ambazo walidhibiti hapo awali katika viunga vya mji huo.

Kulingana na wachambuzi kadhaa, idadi kubwa ya wapiganaji hao nchini Libya walitumwa na Uturuki kusaidia vikosi vya Fayez al Sarraj. Wapiganaji hao huko Sabratha, ni kutoka Libya, Syria, Misri na Tunisia. Wanakuja kujiongeza kwenye idadi ya mamia ya wapiganaji walioachiliwa huru katika magereza ya Sabratha na Tripoli na vikosi vya Fayez al Sarraj baada ya kuvitimuwa vikosi vya Khalifa Haftar mwezi Aprili mwaka jana. Wapiganaji wa al Qaida na IS ambao walikimbia kutoka Sirte, Benghazi na Derna, ni miongoni mwa wapiganaji waopiga kambi huko Sabratha.