BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Watu zaidi ya 20 wauawa Mashariki mwa Burkina Faso

Serikali ya Burkina Faso imetoa wito kwa raia wake kuwa makini (picha ya kumbukumbu).
Serikali ya Burkina Faso imetoa wito kwa raia wake kuwa makini (picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO/ISSOUF SANOGO

Watu wasiopungua 20 wameuawa katika mkoa wa Mashariki mwa Burkina Faso. Watu waliojihami kwa silaha ambao hawajajulikana wawaliwapiga raia katika soko la ng'ombe la Namoungou, karibu kilomita 30 kutoka mji wa Fada N'Gourma.

Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa mkoa huo wa Mashariki wameghadhabishwa na tukio hilo lililotokea jana Ijumaa Agosti 7.

Ilikuwa karibu saa sita mchana wakati wauaji walivamia soko hilo la ng'ombe la Namoungou, gavana wa mkoa huo Kanali Saidou Sanou amesema katika taarifa. Wauaji hao "waliwapiga risasi raia". Kulingana na mashahidi, karibu watu 30 wenye silaha wasiojulikana walitumia pikipiki ili kuweza kufika kwenye soko hilo na baada tu ya kuwasili waliwapiga risasi raia kwa maksudi.

Soko hilo ni soko pekee la ng'ombeambalo lilikuwa likifanya kazi, kando na lile la Fada, katika mkoa huo wa mashariki, kulingana na mkazi mmoja. "Soko zingine za mifugo zilifungwa kufuatia vitisho au mashambulizi ya mara kwa mara," chanzo chetu kimesema.

Shambulio hili la Ijumaa katika soko la Namoungou ni sawa na lile lililotokea huko Kompiembiga mwezi Mei mwaka huu, mashahidi wamesema.

Waziri Mkuu wa Burkina Faso Christophe Dabiré amesema kughadhabishwa na shambulio hilo. zamewakumbusha wakazi wa mkoa huo juu ya dharura ya kuendelea kuwa makini kila wakati, hasa wakati wa mikusanyiko mikubwa.