DRC-CORONA-ELIMU

Coronavirus: Familia nyingi zalalamikia hali ya maisha wakati shule zikianza tena mashariki mwa DRC

Katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini, wilayani Lubero, wanafunzi walijitokeza kwa asilimia tisini kwa mujibu wa Richard Nyembo wa Nyembo, mkuu wa wilaya hiyo ya Lubero.
Katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini, wilayani Lubero, wanafunzi walijitokeza kwa asilimia tisini kwa mujibu wa Richard Nyembo wa Nyembo, mkuu wa wilaya hiyo ya Lubero. © Justin Makangara pour la Fondation Carmignac

Miezi mitano baada ya kukaa nyumbani kama hatua ya kuepukana na maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona, hatimaye wanafunzi wanaohitimu shule za sekondari na zile za msingi wamerejelea masomo mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Bukavu mkoani Kivu Kusini, wanafunzi wote wa darasa la sita katika shule za sekondari na za msingi walijitokeza kwa wingi jana Jumatatu lakini waalimu wachache ndio walionekana.

Katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini, wilayani Lubero, wanafunzi walijitokeza kwa asilimia tisini kwa mujibu wa Richard Nyembo wa Nyembo, mkuu wa wilaya hiyo ya Lubero.

Baadhi ya wazazi bado wanahofia kuwatuma watoto wao kufuatia kile baadhi wanasema kushindwa kupata barakoa kwa watoto wao, wakati huu familia nyingi zikilalamikia hali duni kiuchumi.