DRC-MAREKANI-FARDC-ULINZI

DRC: Kundi la kwanza la maafisa wa FARDC kupatiwa mafunzo Marekani mwezi Septemba

Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimama karibu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmoja huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018.
Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimama karibu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmoja huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018. © AFP

Makumi ya maafisa wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, FARDC, wanatarajia kwenda nchini Marekani kwa mazoezi zaidi mwezi Septemba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano yake na Radio Okapi, Balozi wa Marekani nchini DRC Mike Hammer ametangaza kwamba hilo ni kundi la kwanza la maafisa wa FARDC katika mfululizo wa mazoezi yatakayoendelea kwa miaka kadhaa.

"Tumejipanga kuanza mwezi Agosti, lakini itakuwa vigumu kwa sababu ya janga la Covid-19 -. Nina imani kwamba mafunzo hayo yataanza mwezi Septemba. Kutakuwa na maafisa kadhaa ambao wataweza kushiriki. Na tutaweza kuendelea. "Ni kitu ambacho kilifanywa kwa ushirikiano na Wizara ya Ulinzi, " amesema balozi wa Marekani nchini DRC.

" Wizara ya Ulinzi itatuambia ni maafisa gani waliohitimu kufuata mafunzo mbali mbali ambayo zitafanyika kwa miaka mingi. haya ni mafunzo ambayo tulikuwa tuliandaa hapo awali. Lakini ni ni vizuri kuanza tena kwa sababu ya maendeleo ambayo DRC imepiga katika uheshimishwaji wa haki za binadamu, “ ameongeza balozi Mike Hammer.

Tutaangalia lakini natumai kuwa ni programu ambayo tunaweza kufanya kwa miaka yote na mafunzo pia yanaweza kutolewa na wataalam wa Marekani ambao wanaweza kuja nchini DRC na kufanya mafunzo hapa katika shule mbali mbali za jeshi, za FARDC ", amebaini balozi Mike Hammer.