DRC-ITURI-USALAMA

Kumi na Tisa wauawa katika shambulizi la watu wenye silaha Banyali Kilo, DRC

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS

Watu 19 wameuawa na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea kwa mashambulizi ya waasi ya hivi punde katika vijiji vitatu mkoani Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Innocent Madukadala, kiongozi wa eneo la Banyali Kilo ambako mashambulizi hayo yalitekelezwa, anawashatumu waasi wa kundi la Codeco kuhusika katika mauaji hayo.

Kundi la Codeco limeendelea kunyooshewa kidole cha lawama kuhusima na vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na uporaji katika mkoa wa Ituri.

Shirika la Kimatiafa la kutatua migogoro la International Crisis Group katika ripoti yake mwezi uliopita, lilisema tangu mwaka 2017 utovu wa usalama katika mkoa wa Ituri, umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 na maelfu kuyakimbia makwao.