MALI-SIASA-USALAMA

Majaji wa Mahakama ya Katiba wakula kiapo

Mpatanishi wa ECOWAS, Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan na Waziri Mkuu wa Mali, Boubou Cissé, ambaye upinzani unaomba ajiuzulu.
Mpatanishi wa ECOWAS, Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan na Waziri Mkuu wa Mali, Boubou Cissé, ambaye upinzani unaomba ajiuzulu. Press Service of Prime Ministry/Handout via REUTERS

Majaji wapya katika Mahakama ya Kikatiba wameapishwa nchini Mali, ikiwa ni mojawapo ya hatua ya kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa ambao umekuwa ukiendelea nchini humo kwa miezi kadhaa sasa.

Matangazo ya kibiashara

Hafla hiyo ilihudhuriwa na rais Ibrahim Boubacar Keita, na viongozi wa mashirika ya kiraia baada ya shinikizo la kufanyika kwa uteuzi huo mpya.

Jumuiya ya nchi za Afrika Magharobi ECOWAS imekuwa katika mstari wa mbele kutatua mzozo huo wa kisiasa na kuwarai wapinzani kushirikiana na rais Keita katika serikali ya pamoja.

Mwanasiasa wa upinzani mwenye ushawisi mkubwa nchini mali, Imam Mohamoud Dicko, aameilaumu Ufaransa kwa kuingilia hali ya kisiasa nchini humo.

Hivi karibuni shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilivishutumu vikosi vya usalama nchini Mali kwa kuhusika katika ukandamizaji na umwagaji damu" uliowalenga waandamanaji mwezi uliopita wakitaka kujiuzulu kwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta.

Rais Ibrahim Boubakar Keita ambaye amesalia na miaka mitatu tu katika muhula wake wa mwisho, anakabiliwa na shinikizo za kutaka ajiuzulu tangu mwanzoni mwa mwezi Juni.

Umaarufu wake umeshuka kutokana na madai ya ufisadi yanayoizonga serikali yake huku mzozo wa wapiganaji wa Kiislamu wenye itikadi kali ukiendelea kuitia doa serikali yake.

Wito wa kumtaka rais huyo ajiuzulu umeongezeka baada ya maandamano ya hivi karibuni kujibiwa vikali na vikosi vya usalama, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 12.