COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Upinzani wafutilia mbali hatua ya rais ouattara kuwania muhula wa tatu

Rais wa Cote d’ Ivoire Alassane Ouattara wakati wa mkutano wa kamati ya siasa ya chama cha RHDP Julai 29, 2020 huko Abidjan.
Rais wa Cote d’ Ivoire Alassane Ouattara wakati wa mkutano wa kamati ya siasa ya chama cha RHDP Julai 29, 2020 huko Abidjan. REUTERS/Luc Gnago

Wafuuasi wa upinzani wamekuwa wakiandamana karibu na makao makuu ya Tume ya Uchaguzi jijini Abidjan, nchini Cote d’ Ivoire, kushtumu hatua ya rais Alassane Ouattara kuwania urais kwa muhula wa tatu mweezi Oktoba.

Matangazo ya kibiashara

Wapinzani wa rais Outtara wameapa kutoacha shinikizo hizo wakisema hatua ya rais huyo ni kinyume cha katiba ya taifa hilo, suala ambalo serikali inasema kinachoendelea ni kitu cha kawaida wakati huu wa kisiasa.

Wiki jana rais wa Cote d’ Ivoire Alassane Ouattara, mwenye umri wa miaka 78, aliweka wazi msimamo wake kuwa atagombea kwa muhula wa tatu, hatua ambayo imekuja baada ya kifo cha aliyekuwa waziri wake mkuu Amadou Gon Coulibaly Julai 8.

Ouattara amefikia uamuzi huo baada ya kushinikizwa na chama chake, wabunge kutoka chama chake na taasisi mbalimbali katika chama cha RHDP kumtaka apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao, baada ya kifo cha waziri mkuu Amadou Gon Coulibaly hivi karibuni ambaye alikuwa mrithi wake.

Miezi michache iliyopita, rais wa Cote d'Ivoire alisema hatowania katika uchaguzi wa urais ujao na kuachia nafasi kwa kizazi kipya kuliendeleza taifa hilo la Afrika, lakini kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly ambaye alikuwa aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama tawala katika uchaguzi wa urais, kilibadili hali ya mambo.