SOMALIA-USALAMA

Watu 19 waangamia katika majibizano ya risasi Mogadishu

Gereza Kuu la Mogadishu, mwaka 2013.
Gereza Kuu la Mogadishu, mwaka 2013. AU UN IST PHOTO / Tobin Jones

Wafungwa 15 na askari 4 wameuawa katika majibizano ya risasi katika gereza moja mjini Mogadishu, Somalia. Tukio hilo lilitokea Jumatatu Agosti 10.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya usalama nchini humo vinabaini kwamba watu wanaoshukiwa kuwa wafungwa wa kundi la Al - Shabab waliwafyatulia risasi walinzi wa gereza baada ya kujaribu kutoroka kutoka gereza hilo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Jeshi la Magereza limesema makabiliano hayo yalisababisha vifo vya watu 19 na wengine 8 kujeruhiwa.

Lakini vyanzo vingine vinasema milipuko ya magruneti ilisikika karibu na jela hilo. Vyanzo kadhaa mjini Mogadisho vinabaini kwamba silaha hizo ziliingizwa katika jela hilo siku za hivi karibuni.

Serikali ya Somalia imeanza kuchunguza tukio hilo hasa jinsi ya wafungwa hao walivyopata silaha.

Wakati huo huo polisi inasema kuwa iliwachukua takriban masaa mawili kuwazingira wanamgambo hao na kutuliza hali.

Hata hivyo kuna baadhi ya taarifa ambazo zinadai kuwa mfungwa mmoja wa Alshabab alifanikiwa kutoroka gerezani humo.

Uchunguzi umeanzishwa kubaini mazingira ya shambulio hilo.