MSUMBIJI-Al SHABAB-USALAMA

Msumbiji: Wanamgambo wa Al Shabab wavamia bandari ya kimkakati ya Mocimboa da Praia

Mocimboa da Praia, mji ambako kwa sehemu kubwa wanatoka viongozi wa waasi, pia ni eneo la kimkakati kwa wanajihadi wao, linapatikana kilomita sitini kutoka maeneo ya gesi asilia inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 60.
Mocimboa da Praia, mji ambako kwa sehemu kubwa wanatoka viongozi wa waasi, pia ni eneo la kimkakati kwa wanajihadi wao, linapatikana kilomita sitini kutoka maeneo ya gesi asilia inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 60. ADRIEN BARBIER / AFP

Hii ni hatua mpya ya kundi la wapiganaji la Al Shabab lenye mafungamano na kundi la Islamic State, ambao wanaendelea kusonga mbele katika jimbo la Cabo Delgado, kaskazini mwa nchi Msumbiji.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa kundi hilo wamedhibiti bandari ya kimkakati ya Mocimboa da Praia, karibu na eneo muhimu sana lenye gesi asilia.

Mapigano kati ya wanamgambo hao na vikosi maalum vya Msumbiji yalidumu siku kadhaa kabla ya wanajihadi hao kudhibiti eneo hilo. Bandari ya Mocimboa da Praia hatimaye iko mikononi mwa waasi hao tangu Jumatano alfajiri. Kulingana na vyombo vya habari nchini Msumbiji, jeshi halikuwa na vifaa vya kustosha kwa kukabiliana na shambulizi la waasi hao na helikopta za kivita zilikuwa mbali kwa kuweza kutoa msaada kwa kikosi hicho.

Hii ni mara ya nne tangu 2017 kundi la Al Shabab kujaribu kudhibiti eneo la Mocimboa da Praia.

Kwa mujibu wa Eric Morier-Genoud, mtafiti kuhusu nchi ya Msumbiji katika Chuo Kikuu cha Belfast, shambulio hili ni ushindi mkubwa kwa kundi la Al shabab, kwa sababu usalama uliimarishwa na vikosi maalum. Siku chache zilizopita, kundi la Al shabab lilitangaza kwamba linajipanga kudhibiti eneo hilo ili kulifanya mji mkuu wao.

Mocimboa da Praia, mji ambako kwa sehemu kubwa wanatoka viongozi wa waasi, pia ni eneo la kimkakati kwa wanajihadi wao, linapatikana kilomita sitini kutoka maeneo ya gesi asilia inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 60.