UFARANSA-NIGER-USALAMA

Niger: Miili ya wafanyakazi sita wa shirika la misaada ya binadamu kuwasili Paris Ijumaa

Hifadhi ya wanyama ya Kouré ambapo wafanyikazi sita wa shirika la misaada ya kibinadamu, raia Ufaransa na raia wawili kutoka Niger waliuawa.
Hifadhi ya wanyama ya Kouré ambapo wafanyikazi sita wa shirika la misaada ya kibinadamu, raia Ufaransa na raia wawili kutoka Niger waliuawa. REUTERS/Tagaza Djibo

Miili ya wafanyakazi sita wa shirika la misaada ya kibinadamu, raia wa Ufaransa itawasili Ijumaa, Agosti 14 kwenye uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris. Itawasili kabla ya kumi alaasiri.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex anatarajia kuongoza hafla ya kupokea miili hiyo, ambapo watakuepo ndugu jamaa na marafiki wa wahanga hao kwa kutoa heshima ao za mwisho.

Watu wanane - Wafaransa sita na raia wawili wa Niger - waliuawa na watu wenye silaha ambao walikuja kwa pikipiki katika eneo la Kouré, Kusini Magharibi mwa Niger, eneo linalojulikana kama hifadhi ya mwisho ya Twiga huko Afrika Magharibi.

Haijulikani ikiwa sherehe pia zimepangwa kufanyika nchini Niamey kutoa heshima za mwisho kwa wafanyakazi sita wa kibinadamu wa Ufaransa, lakini pia kutoa heshima za mwisho kwa raia wawili wa Niger ambao waliandamana nao, na kuuawa Jumapili, Agosti 9.

"Majambazi wenye silaha waliokuwa katika magari ndio walihusika na vifo vya raia hao katika eneo la kitalii la Kouré. Eneo hili ni hifadhi ya Twiga, Twiga wa mwisho katika Afrika Magharibi. Tumeanzisha uchunguzi na tumeanza pia kuwasaka majambazi hao katika eneo hilo. Tuna huzuni mkubwa, na ni tukio la kusikitisha kwa kweli. Ktika siku za hivi karibuni, tulikuwa katika hali ya utulivu, tumeshtushwa na tukio hilo, inauma kwa kweli, " alisema Gavana wa mkoa wa Tillabéri akihojiwa na Charlotte cosset.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Niger Mahamadou Issoufou waliapa kuendelea na vita dhidi ya makundi ya kijihadi hadi pale watahakikisha makundi hayo yametokomezwa.