DRC-UCHUMI

Mgomo wasitishwa katika sekta ya mafuta kusini na mashariki mwa DRC

Moja ya mitaa huko Lubumbashi, mkoa wa Haut-Katanga, DRC.
Moja ya mitaa huko Lubumbashi, mkoa wa Haut-Katanga, DRC. JUNIOR KANNAH / AFP

Wafanyabiashara katika sekta ya mafuta katika ukanda wa kusini na mashariki mwa DRC wamesitisha mgomo wao tangu Jumatano wiki hii, baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Serkali ya Kinshasa imetoa jibu kwa madai yao. Kwa sasa bei ya lita moja ya mafuta aina ya petroli imepanda kwa kiwango cha 24%, jambo ambalo si rahisi kwa wanunuzi.

Mazungumzo kati ya Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilukamba na ujumbe wa wafanyabiashara katika sekta ya mafuta yalidumu siku mbili jijini Kinshasa.

Pande zote mbili zimefikia makubaliano hasa kuhusu bei ya petroli. Sasa lita moja ya mafuta itauzwa senti 93 badala ya 75, bei iliyokuwa ikiuzwa hapoa awali.Beyi imependa kwa kiwango cha 24%.

“Mgomo hausaidii chochote, bali unasababisha tu uchumi kudidimia. Kwa hiyo Waziri mkuu ametuahidi mengi baada ya kutusihi tulegeze msimamo, ” amesema Albert Yuma kiongozi wa muungano wa vyama vya wafanyabiashara.

Bei ya lita moja ya petroli mitaani ilikuwa ikiuzwa dola 2 za kimarekani.