COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Côte d’Ivoire: Baada ya machafuko huko Daoukro, pande hasimu zatoa wito wa utulivu

Huko Abidjan, vijana waandamana wakipinga Alassane Ouattara kuwania kiti cha urais, hata hivyo wamekabiliana na polisi, Agosti 13, 2020.
Huko Abidjan, vijana waandamana wakipinga Alassane Ouattara kuwania kiti cha urais, hata hivyo wamekabiliana na polisi, Agosti 13, 2020. Issouf SANOGO / AFP

Mamlaka nchini Côte d’Ivoire imetoa ripoto inayohusiana na machafuko yaliyoikumba nchi hiyo tangu Jumatatu wiki hii. Kulingana na polisi ya kitaifa, machafuko hayo yalisababisha vifo vya watu 3 kote nchini (2 huko Daoukro, 1 katika mji wa Bonoua), na watu kadhaa walijeruhiwa, na uharibifu mkubwa uliripotiwa.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo kadhaa vyenye kuaminika, kwa mji wa Daoukro pekee, watu 113 wamejeruhiwa tangu Jumatatu wiki hii, wengi wao wana majeraha ya risasi na visu au mapanga. Kwa jumla ya majeruhi 113, 21, 21 peke waliripotiwa Alhamisi wiki hii.

Wakati huo huo sheria ya kutotoka nje kwa muda wa siku tatu imetangazwa tangu Jumatano wiki hii. Na vikosi vya usalama vimewekwa kila majala kwa kuzuia maandano ya upinzan

Chama tawala cha RHDP kimetoa wito kwa wafuasi wake kuwa watulivu, kikishtumu upinzani kuhusika na machafuko hayo.

Uchunguzi umeanzishwa ili kubaini wahusika na kujua ikiwa machafuko hayo yalipangwa.