ANGOLA-UCHUMI

Mtoto wa kiongozi wa zamani wa Angola Dos Santos ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela

Jose Filomeno dos Santos, mtoto wa rais wa zamani wa nchiyo, Eduardo Dos Santos., ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela.
Jose Filomeno dos Santos, mtoto wa rais wa zamani wa nchiyo, Eduardo Dos Santos., ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela. REUTERS

Mahakama ya Angola imemhukumu Jose Filomeno dos Santos, mtoto wa kiongozi wa zamani wa nchiyo, Eduardo Dos Santos, kifungo cha miaka mitano jela kwa kuhusika kwake katika kesi kubwa ya ufisadi, shirika la habari la Ureno Lusa limeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa zamani wa mfuko wa taifa la Angola, Jose Filomeno dos Santos, yeye na washtumiwa wenzake wamepatikana na hatia ya kupitisha mlango wa nyuma dola Milioni 500 na kuzihamishia kwenye akaunti ya raia wa Suisse jijini London.

Baba yake aliondoka madarakani mnamo mwaka 2017 baada ya miaka 38 akiwa madarakani, na nafasi yake kuchukuliwa na Joao Lourenço. Rais huyo mpya wa taifa hilo lililokuwa chini ya ukoloni wa Ureno, tangu aiingilie madarakani amekuwa akiwabana washirika wa mtangulizi wake waliokuwa madarakani.

Hivi karibuni Joao Lourenço alimfuta kazi binti ya kiongozi huyo wa zamani wa Angola, Isabel dos Santos, ambaye alikuwa mkuu wa shirika la mafuta la serikali, Sonangol.

Ripoti ya mwezi Desemba 2019, kuhusu "Luanda Leaks" - maelfu ya hati zilizomshtumu kwa matumizi mabaya - zilidhoofisha hali yake na alitangaza Jumanne kuondoka kwenye bodi ya wakurugenzi wa Unitel, kampuni kuu ya simu iliyopo nchini Angola, kumfanya kuwa katika "hali ya mizozo ya kudumu".