AFRIKA-WHO-CORONA-AFYA

WHO: Maambukizi zaidi yanaendelea kushuhudiwa barani Afrika

Ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona vinaendelea kuripotiwa barani Afrika.
Ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona vinaendelea kuripotiwa barani Afrika. NEXU Science Communication/via REUTERS

Shirika la afya duniani WHO linasema, bara la Afrika litaendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona wakati huu nchi nyingi zinapoanza kufungua mipaka yake na maisha kuanza kurejea taratibu, katika bara hilo ambalo lina maambukizi zaidi ya Milioni Moja.

Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC kimesema kinakuja na mfumo wa pamoja wa nchi za Afrika kuwa na utaratibu wa kuwapima wasafiri.

Hayo yanajiri wakati wiki ijayo, nchi saba za Afrika zitaanza kufanya vipimo vya kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona, kulingana na kituo cha Afrika cha kudhibiti magonjwa (CDC).

"Liberia, Sierra Leone, Zambia, Zimbabwe, Cameroon, Nigeria pamoja na Morocco ndio mataifa ya kwanza ya Afrika ambayo yamejidhatiti kufanya vipimo hivyo, kiongozi wa CDC John Nkengasong ameeleza.

Kufikia sasa idadi ya visa vya maambukizi imepindukia Milioni 20.9 duniani wakati idadi ya vifo ikifikia 756,000, baada ya vifo 6,968 kuthibitishwa.