MALI-UN-MAUAJI-USALAMA

Mauaji ya Ogossagou nchini Mali: Ripoti ya UN yawatia hatiani maafisa wakuu

Kijiji cha Ogossagou katikati mwa Mali.
Kijiji cha Ogossagou katikati mwa Mali. RFI

Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mali wamewasilisha ripoti yao kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Ijumaa (Agosti 14). Ripoti hiyo, ambayo bado haijatolewa hadharani lakini RFI imeweza kupata kopi, inatuhumu maafisa wakuu wa Mali kuzuia mchakato wa amani, ulioanzishwa tangu mwaka 2015.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa zamani wa Jeshi na mkurugenzi wa sasa wa Usalama wa taifa ni miongoni mwa maafisa hao wanaonyooshewa kidole cha lawama na wataalamu hao.

Mauaji ya pili katika kijiji cha Ogossagou yangeweza kuzuiwa na wanajeshi wa Mali, wataalam wa UN wanasema katika ripoti ya ndani. Siku hiyo, Februari 14, 2020, kulingana na ripoti hii, wanamgambo wa Dogon walishambulia kijiji cha Fulani. "Waathiriwa walitafutwa hadi msituni, baadhi walikatwa na mapanga na wengine walikatwa vichwa. Jumla, raia 35 waliuawa na 19 bado wamekosekana mpaka sasa.

Ripoti hiyo inamshutumu Jenerali Kéba Sangaré, mkuu wa zamani wa jeshi la nchi kavu na wakati huo alikuwa anaongoza jimbo la kati.

Kama inavyothibitishwa na mpango unaochukuliwa na usalama wa taifa. Mnamo Aprili 2019, Mamlaka ya Malesia ilitoa shinikizo kwa serikali ya Niger kuwaachilia watu wanaounda mtandao wa madawa ya kulevya. Ulinzi ulioahidiwa na idara za usalama za Mali baada ya kukubali kutoa malipo ya kila mwezi "angalau hadi Julai 2018" inasema ripoti hiyo. Pesa hizo zilitolewa na Mohamed Ould Mataly, mbunge nchini humo na mjumbe wa kundi la watu wenye silaha, linalounga mkono serikali, ambaye yuko chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa, na kukabidhiwa Jenerali Moussa Diawara, mkurugenzi wa sasa wa usalama wa taifa Mali na naibu wake anayesimamia kitengo kinachopambana dhidi ya ugaidi , Kanali Ibrahima Sanogo.